Simulizi: JIRANI KAMA JIRANI! Imeandikwa na: Abyas Mzigua Sehemu ya pili ILIPOISHIA: Mke wangu aliondoka nyumbani. Akaniacha mwenyewe. Mchana jirani yangu akaja na kuniletea chakula, pamoja na kujitahidi kukikataa kwa kumueleza nimekwisha kushiba, bado alinilazimisha na kuniambia nikihifadhi nitakula usiku. Hapo sikuweza kumpinga. Sasa tuendelee! Kama ambavyo niliwaeleza, lile poti la chakula nililipokea na kuliingiza ndani. Nikaliweka mezani na kurejea kwenye usingizi wangu. Nilikuja kushtuka kagiza kanakaribia kuingia. Nikagundua kuwa usingizi wangu ulikuwa ni mrefu sana. Ni kweli nilichoka, mno. Usiku wa jana yake sikuwa nimepata usingizi wa kutosha. Nilikuwa ninafanya kazi ya kumbembeleza mwanamke ambaye hakuwa tayari kunisikiliza. Chipsi sio chakula kabisa jamani! Yani niliamka njaa imenibana mno. Tumbo jeupeee, linadai chakula tu. Moja kwa moja nikaenda katika meza. Nikalifungua lile poti. Ambalo tangu nilivyolipokea...